Album Cover Wewe ni Mungu

Wewe ni Mungu

Kwaya ya Mt. Kizito Makuburi

6

Sikia aa sikia Bwana,

Sikia aa sikia Bwana sauti yangu

Sikia aa sikia leo

Sikia aa sikia Bwana sauti yangu.

Hii sauti inabeba hisia zangu

Zilizomo moyoni mwangu sikia Bwana sauti yangu

Naeleza furaha niliyo nayo

Na hamu ya kukushukuru sikia Bwana sauti yangu.

Nakufunulia moyo wangu uko wazi,

Nakumiminia, sifa na tenzi Mwenyezi,

Napiga kelele usikie Bwana sauti yangu

Sikia aa sikia Bwana (Mungu we)

Sikia aa sikia Bwana sauti ya moyo,

Moyo,moyo, wangu moyo, moyo, moyo ha ha-

Nimejua ya kwamba - wewe ni Mungu kila wakati

Naona wazi kwamba - wewe ni Mungu kila wakati

Kwenye furaha - wewe ni Mungu kila wakati

Na kwenye magumu bado- wewe ni Mungu kila wakati

Haupungui neno - wewe ni Mungu kila wakatii

Hukutaka raha zinipe kiburi -

Aeee eee ukanipimia.

Na taabu ziliponishambulia - -

Ukafungua (Bwana) mlango nikatoka salama.

Nimejua ya kwamba - wewe ni Mungu kila wakati

Naona wazi kwamba - wewe ni Mungu kila wakati

Kwenye furaha - wewe ni Mungu kila wakati

Na kwenye magumu bado- wewe ni Mungu kila wakati

Haupungui neno - wewe ni Mungu kila wakatii

Na vipaji ona hukunipa vyote -

Aaee eee ukanipimia.

Ingawaje nilipoweka juhudi -

Ukafungua(Bwana) mlango nikatoka salama.

Nimejua ya kwamba - wewe ni Mungu kila wakati

Naona wazi kwamba - wewe ni Mungu kila wakati

Kwenye furaha - wewe ni Mungu kila wakati

Na kwenye magumu bado- wewe ni Mungu kila wakati

Haupungui neno - wewe ni Mungu kila wakatii

Sikuumbwa msafi kama ulivyo,

Aaee eee ukanipimia.

Hata hivyo dhambi iliponisonga,

Ukafungua (Bwana) mlango nikatoka salama.

Nimejua ya kwamba - wewe ni Mungu kila wakati

Naona wazi kwamba - wewe ni Mungu kila wakati

Kwenye furaha - wewe ni Mungu kila wakati

Na kwenye magumu bado- wewe ni Mungu kila wakati

Haupungui neno - wewe ni Mungu kila wakatii

Yeyeyeye yeyeyeyeye yeyeyeyeyeeeeee

Nakuja nimebeba sifa kukuzungushia

Nakuja ninaimba wimbo watu wakutukuze

Nakuja nimebeba sifa kukuzungushia

Maana utukufu ni wako milele na milele.

Nakuja nimebeba shangwe, na chereko

Nakuja nimebeba kinanda watu wakuimbie-

Nakuja nimebeba sifa kukuzungushia

Maana utukufu ni wako milele na milele.

Nakuja nimebeba sifa kukupamba

Nakuja nimebeba maua jama watu wakutukuze-

Nakuja nimebeba sifa kukuzungushia

Maana utukufu ni wako milele na milele.

Milele na milele, milele na milele,

Milele na milele,milele ni Mungu wa pekee...

* (Bass) Wewe ni Mungu, wewe ni Bwana,

We ni mwema, utabaki Mungu

* (Tenor) wewe ni wa kwanza ni Mungu weee, wewe ni wa mwisho eee

Unaitwa Alfa ni Mungu wee, wewe ni Omega eee

Lagu lain oleh Kwaya ya Mt. Kizito Makuburi